Habari Mseto

Mitandao lawamani kwa mimba za mapema

November 12th, 2018 1 min read

Na SAMMY KIMATU

MIMBA nyingi miongoni mwa wanafunzi zinachangiwa na mitandao, kiongozi wa kanisa amesema.

Aidha, mhubiri huyo alilaumu pia viongozi wenzake wa makanisa kwa kukosa kuwajibika kuwafunza waumini na wananchi kwa jumla umuhimu wa kujiepusha na mimba za mapema na sizizotakikana.

Mkuu wa kanisa la Oasis of Grace (OOGC), Askofu George Kamunya alisema hayo jana wakati wa ibada ya Jumapili katika makao makuu ya kanisa hilo jijini Nairobi.

“Watoto wengine wanatoka katika familia zinazosimamiwa na akinamama. Hapa msichana anaona vile mamake huleta mwanamume katika nyumba juu anawalisha na kuwalipia karo kisha anaiga wafanyayo,” Bw Kamunya akasema.

Isitoshe, aliongeza kwamba matamshi ya wanasiasa katika mikutano ya hadhara pia lachangia suala hili.Aliomba pia vilabu wanafunzi hujiunga navyo shuleni zipigwe darubini ili kubaini yanayoendeshwa wakati wa mikutano.

“Kuna umuhimu wa somo la jinsia na usafi wa mwili kuwekwa katika mtahala shuleni ili iwe kama somo kuanzia darasa la sita kwenda juu,” askofu Kamunya akaongeza.Kupitia hayo, alisema wanafunzi watakuwa wanajielewa na visa vya aina hii bila shaka zitapungua.