MIZANI YA HOJA: Jipangie jinsi ya kuendelea kuishi vizuri wakati wa mtihani na baada ya mtihani

MIZANI YA HOJA: Jipangie jinsi ya kuendelea kuishi vizuri wakati wa mtihani na baada ya mtihani

NA WALLAH BIN WALLAH

MITIHANI ni sehemu ya maisha ya kila siku kwa mwanadamu.

Kuna mitihani sampuli nyingi sana maishani kama vile mitihani ya kiuchumi na gharama ya maisha; mitihani ya afya na misukosuko ya bughdha za maradhi mwilini; mitihani ya kuhangaika kutafuta pesa ndipo mtu ale ashibe, avae vizuri na alale unono.

Lakini mtihani mkubwa uliozoeleka na kutambulika zaidi maishani ni wa masomo shuleni kama vile walivyo sasa vijana wetu wanaopambana na mitihani yao.

Hapo ndipo ninapowakumbusha kwamba kuishi ni mtihani. Maisha ni mtihani. Unapofanya mtihani wa shuleni sharti pia ujipangie utaratibu na ratiba yako ya kufuata kila siku ili ujue wakati unapopaswa kudurusu kwa ajili ya kila karatasi ya inayofuata.

Pia ujue wakati utakapofanya shughuli nyingine za maisha kama vile kula, kuoga, kucheza, kupumzisha ubongo wako na muda wa kulala. Ni muhimu kutekeleza kila jambo na kila jukumu kwa wakati wake maalumu.
Jambo jingine muhimu zaidi ni kujiuliza utafanya nini au ufanye nini baada ya kumaliza mtihani wako wa mwisho shuleni.

Maisha

Kumbuka kukamilisha kufanya mtihani wa masomo shuleni si mwisho wa maisha wala mwisho wa kusoma vitabu ili kwamba huwezi kufanya shughuli zozote tena baada ya mtihani!

Jipangie maisha ujue kila siku utafanya nini? Utalala saa ngapi? Utaamka saa ngapi na utafanya kazi zipi za kuyaendeleza maisha yako vizuri bila uvivu wa kukaa bure ama kuzurura tu shelabela mitaani!

You can share this post!

KOMBE LA DUNIA FIFA 2022: Argentina watinga hatua ya 16-bora

NGUVU ZA HOJA: Ufala aliouzungumzia Rais Ruto unaweza...

T L