Mjakazi akiri kuiba mali ya mwajiri wake

Mjakazi akiri kuiba mali ya mwajiri wake

NA JOSEPH NDUNDA

MJAKAZI alifikishwa katika Mahakama ya Kibera, Nairobi akikabiliwa na shtaka la kuiba vito vya thamani ya Sh573,411 kutoka kwa mwajiri wake.

Bi Caroline Nabwire alikiri kwamba katika siku tofauti kati ya Januari 31 na Februari 28, 2021, mtaani Parklands, jijini Nairobi, aliiba aina tofauti ya vito, mali ya Ventrapragada Nikhil.

Kulingana na shtaka dhidi yake, alipata mali hiyo akiwa mfanyakazi wa nyumbani wa mlalamishi.

Bi Nambwire aliyeshtakiwa mbele ya Hakimu Mkuu Mkazi, Renee Kitangwa, anatarajiwa kuhukumiwa leo Jumatano.

You can share this post!

Washukiwa 6 wa wizi wa mabavu wanyakwa Bungoma

Wapigakura wafafanulia wanasiasa matakwa yao

T L