Habari

Mjerumani anayedaiwa kuchafua watoto wadogo azuiliwa siku 21

May 5th, 2020 1 min read

Na RICHARD MUNGUTI

MZEE anayedaiwa kuwachafua, kuwabaka na kuwalawiti wavulana wenye umri mdogo atakaa rumande kwa siku 21 kuhojiwa na kuchunguzwa zaidi.

Thomas Scheller, mahakama imeamuru asalie mikononi mwa polisi hadi Mei 30.

Alitiwa mbaroni katika lango la afisi za ubalozi wa Uherumani akiwa na “windo lake” mvulana mwenye umri wa miaka 15 aliyemsafirisha kutoka Kisumu mwezi Aprili.

Alikamatwa na polisi wanaolinda haki za kina mama na watoto kutoka idara ya uchunguzi wa jinai mnamo Mei 4 2020.

Hakimu mkazi Bi Carolyne Muthoni Nzibe ameelezwa Scheller amekuwa akisakwa na polisi tangu Aprili 4, 2020 alipokwepa mtego wa polisi Kaunti ya Kwale.

Afisa anayechunguza kesi hiyo Lawrence Okoth amefichua kwamba Mjerumani huyo alikuwa amejifungia ndani ya lojing’i eneo la Ngara, Nairobi alipokuwa anamtendea unyama mvulana huyo wa shule moja ya msingi ya Kisumu.

Polisi walikuwa wamemleta mvulana huyo kortini kuomba agizo azuiliwe na idara ya watoto.

Okoth amedokeza kwamba mshukiwa huyo anatakiwa kufunguliwa mashtaka ya kulangua watoto, ubakaji, unajisiĀ  na uundaji wa filamu za ngono anazouzia mshukiwa mwingine Ujerunani.

“Scheller huchukua video za watoto wa umri mdogo wakishiriki ngono kisha anazipeperusha kwa mshirika wake nchini Ujerumani,” Okoth amesimulia hayo mahakamani leo Jumanne.

Ameongeza kusema polisi wamekuwa wakimwinda na “bahati ilisimama Jumatatu alipotiwa nguvuni akijaribu kuingia ubalozi wa kwao kujificha.”

Mahakama imejuzwa Scheller amekuwa akijihusisha na ukiukaji wa haki za wasichana na wavulana wa umri mdogo.

Hakimu amekataa kuruhusu ombi la Scheller azuiliwe soku 60 akisems “Polisi wanaweza kukamilisha uchunguzi katika muda wa siku 2.”

Hata hivyo alimweleza Okoth arudi tena kortini baada ya siku hizo 21 kueleza ikiwa amekamilisha uchunguzi .

” Ikiwa hautakuwa umekamilisha uchunguzi korti itakuongeza muda zaidi.Polisi haizuiliwi na sheria za Kafyu. Mnaruhusiwa kusafiri popote,”Nzibe alinweleza Okoth.

Mahakama ilielezwa Scheller ali

amekuwa akichukua picha za watoto wakisjhiriki ngono Kwale na kuziuza kwa mamilioni ya pesa Ujerumani.