Mjukuu wa Moi aandamwa na mke waliyetalikiana agharimie zaidi malezi ya watoto

Mjukuu wa Moi aandamwa na mke waliyetalikiana agharimie zaidi malezi ya watoto

NA JOSEPH OPENDA

MJUKUU wa marehemu Daniel Moi, Bw Collins Kibet, bado anakumbwa na masaibu baada ya mkewe waliyetengana kukata rufaa akidai posho ya juu kuliko Sh1.5 milioni za kutunza watoto ambazo mahakama iliagiza alipwe kila mwaka.

Bi Gladys Jeruto Tagi kwenye rufaa aliyowasilisha katika Mahakama Kuu ya Nakuru, anataka uamuzi wa Hakimu Mwandamizi Benjamin Limo ubadilishwe ili Bw Collins Kibet Moi ashurutishwe kubeba mzigo mkubwa zaidi wa kutunza watoto wao wawili walio na umri wa miaka 11 na 9. Mzigo utapanda hadi Sh6 milioni.

Katika uamuzi aliotoa Juni 2, Bw Limo aliagiza Bw Kibet kukidhi mahitaji ya elimu, matibabu na kugawana gharama ya burudani na Bi Tagi, gharama ya jumla ikiwa Sh1.5 milioni kwa mwaka.

Hakimu aliagiza Bi Tagi kushughulikia mahitaji yaliyosalia.

Bi Tagi alikuwa ameomba korti imshurutishe Bw Kibet kumlipa Sh200,000 kila muhula wa elimu, Sh200,000 za bima ya matibabu na Sh100,000 za burudani.

Aidha, alitaka Sh100,000 za chakula, Sh150,000 za matumizi yake binafsi, Sh100,000 za mavazi, na Sh50,000 za mjakazi.

  • Tags

You can share this post!

Fernandinho arejea Brazil kuchezea Athletico Paranaense...

Kiraitu aapa kuangusha Mbunge uchaguzini ubabe kati yake na...

T L