Habari Mseto

Mjukuu wa Moi ataka familia ifanyiwe DNA

February 15th, 2024 1 min read

NA SAM KIPLAGAT

MJUKUU wa aliyekuwa Rais marehemu Daniel Moi (mwanawe Jonathan Kipkemboi Moi), anataka uchunguzi wa DNA ufanywe kwa watoto wote wanaotaka kunufaika na mali ya babake, kabla ya kugawanywa.

Katika ombi lililowasilishwa katika Mahakama Kuu ya Milimani, Bw Clint Kiprono Moi, alisema uchunguzi huo utathibitisha warithi halisi wa mali ya Jonathan, almaarufu JT.

Mwaka jana, mpatanishi alibainisha warithi 19 na ripoti ambayo ilipitishwa na Mahakama Kuu na kuamrisha kwa nyumba nne, kuchagua mtoto mmoja kuwa msimamizi kwa urithi ya mali inayozozaniwa.

“Katika maslahi ya haki na kuwezesha uamuzi wa haraka kwa sababu hii, ni haki kwa watoto halali wa marehemu wathibitishwe,” alisema Bw Kiprono.

Hakimu Maureen Odera baadaye alipitisha ripoti hiyo aliamua kwamba itakuwa ya haki na usawa kw kila nyumba kuwa na uwakilishi.