Habari Mseto

Mkapa aliuawa na malaria – Familia

July 27th, 2020 1 min read

AFP NA FAUSTINE NGILA

Dar es Salaam, TZ

Rais wa zamani wa Tanzania Benjamin Mkapa alikuwa ameugua Maralia na alikufa kwa mshuto wa moyo, familia yake ilisema Jumapili huku ikiondoa madai kwamba alifariki kwa virusi vya corona.

“Mkapa alipatikana na maralia na akalazwa hospitalini kuanzia Jumatano,” mmoja wa watu wa familia Williama Eriko alitaja  kwenye misa ya wafu iliyopeperushwa hewani na televisheni ya kitaifa TBC.

Mkapa aliyeongoza Tanzania kuanzia 1995 hadi 2005, alifariki Ijumaa akiwa na miaka 81 kwenye hospitali ya Dar es Salaam lakini serikali haikutaja  kilichosababisha kifo cha Bw Mkapa.

“Alikuwa anajihisi vizuri Alhamisi na nilikuwa naye mpaka saa mbili usiku,” alisema Eriko.

Rais Magufuli alihudhuria misa hio ya wafu akiwa na naibu rais wake na waziri mkuu kwenye uwanja wa uhuru.

Upizani umeikosoa serikali ya Magufuli kwa kutokuwa na uwazi jinsi wankabiliana na janga la virusi vya corona,huku rais huyo alitangaza kwamba hakuna virusi vya corona nchini Tanzqania huku akiimiza watalii warudi.