Shangazi Akujibu

Mke anataka tuhusishe barobaro fulani kwenye miereka yetu ya chumbani

June 10th, 2024 1 min read

Shangazi;

Vipi shangazi. Huu ni mwaka wa 15 tangu tuoane na mke wangu. Katika muda huu wote tumekuwa shwari. Lakini hivi majuzi ameanza kunishangaza; anajaribu kunishawishi tumhusishe kaka fulani wakati wa tendo la ndoa, eti kuongeza ladha. Hii ni sawa?

Sijawahi sikia jambo kama hilo na bila shaka sio sawa. Mbali na kuhatarisha ndoa yenu, inawaweka kwenye hatari ya kuambukizwa maradhi ya zinaa.

Mke siku hizi amezidi na kidomodomo

Shangazi, kwa miaka miwili ambayo tumeona na mke wangu hatujawahi kukosana. Lakini hivi majuzi amekuwa akinikosea heshima hata mbele ya watu. Ananijibu atakavyo. Asipokoma nitamuacha.

Zungumza naye ili ujue nini kinachomkera. Huenda kuna jambo linamkera na hii ndio njia anayotumia kuwasiliana

Familia yao hainitaki, kisa kabila yangu

Nimekuwa nikichumbiana na kaka mmoja ambaye ananipenda sana. Alikuja kwetu kujitambulisha, nami nikaenda kwao. Tulikuwa hata tunapanga harusi lakini imebidi kuweka mipango kando kwani anasema familia yake hainitaki kwa misingi za kikabila. Nifanyeje?

Kama kaka huyo anakupenda kwa dhati hataacha familia yake iwe na ushawishi mkubwa katika uhusiano wenu. Sio wao wanakuoa, ni yeye.

Bosslady pale kazini ananitaka cha lazima!

Nimeoa na tuko na watoto watatu. Kazini kwangu kuna mwanamke mwenye mamlaka amekuwa akiniandama akitaka tuwe wapenzi. Hata anatishia kuniachisha kazi nikikataa. Nifanyeje?

Hiyo ni dhuluma ya kimapenzi na unapaswa kumuonya. Endapo hatosikia, hauna budi ila kumshtaki katika idara ya maslahi ya wafanyakazi afisini mwenu.