HabariKimataifa

Mke wa zamani wa Nelson Mandela, Winnie Madikizela afariki

April 2nd, 2018 1 min read

Na WANDERI KAMAU

ALIYEKUWA mke wa rais wa kwanza Mweusi wa Afrika Kusini, Nelson Mandela, Bi Winnie Madikizela Mandela ameaga dunia.

Bi Mandela alifariki Jumatatu nchini humo akiwa na umri wa miaka 81.

Kulingana na taarifa kutoka kwa msaidizi wake, Bi Mandela alifariki Jumatatu alasiri baada ya kuugua kwa muda mrefu.

“Alituacha baada ya kuugua kwa muda. Alifariki akiwa usingizini akiwa amezungukwa na jamaa zake,” ikasema taarifa kutoka kwa familia.

Bi Mandela pia atakumbukwa kwa kuwa mkuu wa kampeni za Bw Mandela, wakati aliwania urais. Alipigania uhuru wa Afrika Kusini pamoja na ubaguzi wa rangi almaarufu ‘Apartheid’.

Marehemu alizaliwa mnamo Septemba 26, 1936 ambapo alijitosa siasani ukubwani mwake.