Kimataifa

Mkenya afumaniwa akimbaka ajuza mgonjwa Amerika

October 24th, 2018 1 min read

Na PETER MBURU

MWANAMUME Mkenya wa miaka 44 ametiwa mbaroni Marekani, baada ya kupatikana akimbaka ajuza mgonjwa wa miaka 72.
Bw Thomas Kamau Ng’ang’a ambaye ni muuguzi alipatikana na mhudumu mwenzake wa afya akitekeleza unyama huo hospitalini ndipo akaripotiwa.
Bw Ng’ang’a alikuwa muuguzi katika hospitali ya Lexington Rehabilitation and Healthcare, katika eneo la Richmond, Virginia.
Alipatikana akijilazisha ndani ya ajuza ambaye alikua amefika katika hospitali hiyo kutafuta huduma za afya.
Punde baada ya kukamatwa, mshukiwa alizuiliwa jela ya kaunti ya Henrico ambapo alinyimwa bondi, huku akisubiri kufikishwa kortini Desemba.
Aidha, alifutwa kazi mara moja wakati alipokamatwa.
Nakala za korti zilionyesha kuwa Bw Ng’ang’a ana mke na watoto.