Habari Mseto

Mkenya ajuta kulangua raia watatu wa Uganda

May 24th, 2018 1 min read

Na RICHARD MUNGUTI

RAIA wa Kenya alishtakiwa Jumanne kwa ulanguzi wa binadamu. Alikana mnamo Mei 14 katika mtaa wa  Nairobi West aliwalangua raia watatu wa Uganda.

Shtaka lilisema Bi Agnes Sibaka Komen (pichani) aliwazuia ndani ya nyumba yake Nadunga Rahima , Nabutomo Alizik na Namaloba Annet.

Shtaka la pili lilisema mshtakiwa alikuwa amewawekea kisiri hati zao za usafiri.

Shtaka la tatu lilisema kuwa alikuwa ameweka hati hizo za usafiri kwa lengo la kuwalangua raia hao wa Uganda.

Kesi itasikizwa Mei 29 2018. Mshtakiwa aliachiliwa kwa dhamana ya Sh400,000.

Upande wa mashtaka ulisema kesi hiyo isikizwe mapema kwa vile walalamishi wanahitajika kurudishwa nchini Uganda.