Mkenya azuiliwa Uhispania kwa kugeuka mla watu

Mkenya azuiliwa Uhispania kwa kugeuka mla watu

Na Hilary Kimuyu

POLISI katika mji wa Uhispania wa Seville wanamzuilia mwanamke Mkenya anayedaiwa kuuma na kula vidole viwili vya mwenzake waliyekuwa wakiishi naye chumba kimoja.

Inadaiwa vilevile mshukiwa alijaribu kumnyofoa mhasiriwa viungo vyake vya ndani mbele ya binti yake mwenye umri wa miaka sita. Mwanamke huyo mwenye umri wa miaka ya 45, alikamatwa kuhusiana na mashtaka ya jaribio la kutekeleza mauaji.

Polisi wa Uhispania walisema mshukiwa alidaiwa kumshambulia mhasiriwa wake ambaye ni raia wa Congo, katika chumba kimoja kwenye mji wa kusini wa Seville kwa sababu aliamini “amepagawa.”

Maafisa walipata mshambulizi huyo akiwa juu ya mwanamke mwenzake baada ya kufika upesi chumbani humo kufuatia simu walizopigiwa na majirani waliojawa na hofu.

Iliripotiwa kuwa bintiye mshukiwa alikuwemo chumbani humo aliposhikwa na wazimu.

Kulingana na gazeti moja nchini humo, Diario de Sevilla, mwanamke huyo Mkenya alidaiwa kujaribu kumtoa mhasiriwa wake viungo vyake vya ndani kwa kutumia jiwe alilokuwa amemshambulia nalo kwa kuliingiza kwa nguvu katika sehemu yake ya kuendea haja kubwa.

You can share this post!

CHARLES WASONGA: SGR kuelekea Malaba itapiga jeki biashara

KDF wajengea Waboni shule ya bweni