Habari MsetoSiasa

Mkewe Gideon Moi akataa kazi ya serikali

May 19th, 2019 1 min read

Na PETER MBURU

ZAHRA Moi, mkewe seneta wa Baringo Gideon Moi amekataa uteuzi kuwa mkurugenzi katika Bodi ya Usimamizi wa Muungano wa Hospitali Kenya, ambao unamiliki Nairobi Hospital.

Zahra alikuwa ameteuliwa kwa kazi hiyo lakini akajitetea kuwa ana kazi ya kutosha sasa, na hivyo hawezi kujihusisha na shughuli za bodi hiyo ipasavyo.

Aidha, Zahra alisema kuwa hakutuma maombi ya kupewa kazi hiyo, wala kufika katika mikutano ambayo iliamua ateuliwe.

“Ninajuta kwa kuwa inanibidi nikatae uteuzi wenu. Hii ni kutokana na ukosefu wa muda, kwani ratiba yangu kwa sasa hainiruhusu kujihusisha na shughuli za bodi kwa wakati huu,” akasema, kupitia barua.

Alisema kuwa kwa muda hajakuwa katika hospitali hiyo ya Nairobi, kinyume na habari zilizokuwa zikisambazwa, kuhusiana na kubadilishwa kwa usimamizi katika kituo hicho.