Habari Mseto

Mkewe Kidero apewe ushahidi, EACC yaagizwa

December 10th, 2018 1 min read

Na RICHARD MUNGUTI

MAHAKAMA kuu Jumanne iliiamuru tume ya kupambana na ufisadi nchini EACC imkabidhi mkewe aliyekuwa Gavana wa Nairobi Dkt Evans Kidero nakala za ushahidi ilizotwaa kutoka kwa makazi yake.

Jaji Hedwig Ong’undi aliamuru maafisa waliotwaa nakala za hati kutoka kwa  Dkt Susan Mboya wamrudishie mara moja.

“Dkt Susan Mboya hakuwa anachunguzwa. Maafisa wa EACC walitwaa hati zake kinyume cha sheria,” alisema wakili James Ochieng Oduol anayemwakilisha mlalamishi pamoja na wa wakili James Orengo aliyepia Seneta wa Siaya James Orengo.

Bw Oduol na Bw Orengo walimweleza Jaji Ong’udi kuwa maafisa wa EACC wanamsumbua Susan bure.

Mawakili hao waliomba mahakama iamuru wapelelezi hao na wachunguzi hao wa EACC wakome kumsumbua Susan.

Jaji huyo alielezwa maafisa hao wa EACC hawana ushahidi wowote wanaoweza kutumia kumfungulia mashtaka Susan “ ndipo wakavamia makazi yake na afisi yake kusaka ushahidi.”