Habari Mseto

Mkewe tajiri wa Thika aliyetoweka achunguzwa

October 13th, 2020 1 min read

NA MWANGI MUIRURI

Mke wa tajiri mtajika wa Thika Julius Gitau ambaye ni mwanabiashara anachunguzwa kuhusiana na kupotea kwa mumewe.

Polisi wanasema mwanamke huyo na dereva wake ni washukiwa kwenye tukio hilo huku shughuli ya kutafutwa kwa mwanabiashara huyo ikifikia siku ya 24.

“Wawili hao wanaaminika kuwa na ujumbe  wa alipo mwanabiashara huyo,” mkuu wa polisi wa Gatanga Peter Mucheru aliambia Taifa Leo

“Wawili hao waliripoti kupotea kwa mwanabiashara huyo saa kumi jioni huku wakiandikisha kwamba Bw Gitau alikuwa na miaka 44 lakini tumethibitisha kwamba Bw Gitau alizaliwa mwaka 1976 kumaanisha kwamba alikuwa na miaka 44. Tunashindwa na niaje Bi Wahu hajui miaka ya mumewe,” alisema.

Bi Wahu alisema kwamba walichukua matatu kwenye kituo cha Ndururumo kuelekea Thika kwenda kufungua maduka yao ya jumla.

Walitumia magari ya abiria kwani gari la mwanabiashara huyo halikuwa na mafuta lakini mwenyekiti wa muungano wa wanabiasahara Kiambu Alfred Wanyoike alikanaa madai hayo akisema kwamba “magari yote ya mwanabiashar huyo hayakuwa na kasoro”.

“Madai mkewe kwamba Gitau alikosa mafuta ya gari si ya ukweli wafanyabkazi wake walisema kwamba mwanabiashara huyo hakufika kazini.”

Wahu na Wachira tena waliambia polisi kwamba  Bw Gitau aliendesha gari lake mzee kwenda gymkilomita tau mbali saa tatu na nusu lakini hakuna ushahidi kwamba alienda kwa mazoezi.