MKU yashirikiana na UN kuwajali wanaoishi na ulemavu

MKU yashirikiana na UN kuwajali wanaoishi na ulemavu

Na LAWRENCE ONGARO

SHIRIKA la Umoja wa Mataifa (UN) linatambua juhudi za Chuo Kikuu cha Mount Kenya (MKU) za kuwajali wanaoishi na ulemavu.

Naibu Chansela wa MKU Prof Deogratius Jaganyi, alieleza kuwa kwa ushirikiano wa pamoja na UN, chuo hicho kitaendelea kufadhili watu wanaoishi na ulemavu kwa miaka mitatu mfululizo.

Prof Jaganyi alikuwa akihutubia walimu na wanafunzi mjini Thika mwishoni mwa wiki jana ambapo baadhi ya wanaoishi na ulemavu walinufaika na viti vya magurudumu.

Alieleza ya kwamba hivi karibuni wanapanga kufanya ushirikiano na kikundi cha watu wanaoishi na ulemavu ili wawe na mwelekeo mwafaka wa kuendelea kujitafutia riziki bila usumbufu.

“Chuo hiki kinaedesha kozi kwa wanafunzi kuelewa jinsi wanavyoweza kuelewa idadi ya kikundi hicho cha wanaoishi na ulemavu ili kuwapa mwongozo wa kimaisha na kuafikia malengo yao,” alifafanua msomi huyo.

Alieleza ya kwamba MKU itazidi kufuatilia hali za watu hao ili kuona ya kwamba hawatelekezwi popote walipo.

Chuo hicho, kulingana na Prof Jaganyi, kinataka kuona ya kwamba kikundi hicho kinaedesha shughuli bila kudhulumiwa.

Hafla huyo ilihudhuriwa na wahadhiri kadha wa chuo hicho pamoja na wanafunzi.

Chuo hicho pia kimefungua milango kwa walio na upungufu wa afya kujiunga nacho ili kuendeleza masomo yao.

“Sisi katika chuo hiki hatuna ubaguzi wowote ambapo tunapokea mtu yeyote aliye na ari ya kujiendeleza kimasomo,” alieleza Prof Jaganyi.

Chuo hicho pia kimekuwa na ushirikiano na hospitali ya Thika Level 5 huku wanafunzi wengi wa somo la afya kutoka chuo hicho wakifanya majaribio yao huko.

Wakati huo pia wamekuwa mstari wa mbele kutoa matibabu ya bure kwa wakazi wanaoishi kwenye vitongoji duni kama Kiandutu na Kiang’ombe mjini Thika.

You can share this post!

FA yashtumu tukio la ubaguzi wa rangi dhidi ya Saka, Sancho...

Ford Kenya yakanusha kufanya mazungumzo ya 2022 na Dkt Ruto