Mkufunzi mpya Rangnick hana nia ya kuachilia Man United baada ya kandarasi ya miezi sita

Mkufunzi mpya Rangnick hana nia ya kuachilia Man United baada ya kandarasi ya miezi sita

Na MASHIRIKA

MANCHESTER, Uingereza

KOCHA mpya wa Manchester United Ralf Rangnick amefichua yuko tayari kuendelea kuongoza klabu hiyo hata baada ya kandarasi yake kushikilia kwa miezi sita na nusu itakapokatika Juni.

Mjerumani huyo alisema hayo alipofanya kikao cha kwanza rasmi na wanahabari uwanjani Old Trafford, Ijumaa.

Rangnick alishuhudia mchuano wa mwisho wa kocha Michael Carrick dhidi ya Arsenal mnamo Alhamisi.

Carrick alishikilia wadhifa huo kwa mechi tatu tangu Ole Gunnar Solskjaer atimuliwe.

Rangnick,63, ataanza kazi rasmi wakati United itazuru uga wa Selhurst Park kesho Jumapili kuvaana na Crystal Palace.

Aliratibiwa baadaye jana kukutana na wachezaji waliokosa mchuano wa Arsenal.

Rangnick anafaa kutumikia United kama mshauri kandarasi yake ya kuwa kocha mshikilizi itakapotamatika.

Kocha wa Paris Saint-Germain, Mauricio Pochettino anaaminika kuwa mtu ambaye United inataka kuongoza klabu hiyo kwa muda mrefu, ingawa pia inawatamani Erik ten Hag (Ajax) na Brendan Rodgers (Leicester).

Rangnick alitafutwa na Chelsea mwezi Februari, lakini akakataa ilipotaka kumpa kandarasi ya miezi minne.

You can share this post!

Wanaotapeli kwa jina la mkewe Ruto wasakwa na polisi

Shule zafungwa Addis wanafunzi wavune mazao ya...

T L