Habari Mseto

Mkurugenzi aliyetimuliwa aitaka National Bank imlipe Sh450 milioni

November 2nd, 2018 1 min read

Na BERNARDINE MUTANU

Aliyekuwa mkurugenzi mkuu wa Benki ya National Munir Sheikh Ahmed ameshtaki benki hiyo kwa kumfuta kazi.

Anataka kulipwa Sh453 milioni baada ya kuachishwa kazi Aprili 2016. Aliondolewa kutoka kwa wadhifa wake kwa kudaiwa kughushi habari kuhusiana na akaunti za benki hiyo.

Bw Ahamed anataka kurejeshwa humo kama meneja mkurugenzi na masharti aliyokuwa nayo alipoondoka humo baada ya kufutwa, au kulipwa marupurupu ya miezi 76 ambayo ilikuwa imesalia katika kandarasi yake.

Mkurugenzi huyo wa zamani katika mashtaka aliyowasilisha mbele ya Mahakama ya Uhusiano wa Leba alisema aliondolewa katika wadhifa wake kwa njia haramu kinyume na sheria na kumfanya kuamua kupinga hatua hiyo mahakamani.

Anataka mahakama kutangaza hatua hiyo ya kumwachisha kazi kama ambayo haikufuata sheria, isiyo haki, isiyo na kisheria na makosa, kinyume cha sheria ya leba na Katiba.

Hakimu Bryam Ongaya alimtaka Munir na NBK kufika mahakamani Jumatatu kusikizwa kwa kesi hiyo kati yao.