Mkutano ulituletea ushindi, adai Kane

Mkutano ulituletea ushindi, adai Kane

NA MASHIRIKA

LONDON, Uingereza

NAHODHA Harry Kane amesema mkutano wa wachezaji ulisaidia timu hiyo kurejea katika kiwango chake bora ambacho kilichangia katika ushindi wao wa 1-0 dhidi ya Fulham ugenini Craven Cottage, Jumatatu usiku.

Kane alifunga bao hilo la ushindi na kufikia rekodi ya Jimmy Greaves ya kufungia klabu hiyo mabao 266.

Ulikuwa ushindi wa pili kwa Spurs katika mechi sita, baada ya mapema mwezi huu kuchapwa 2-0 na Arsenal kabla ya kukung’utwa 4-2 na Manchester City.

Ushindi huo kadhalika umeirejeshea Spurs matumaini ya kumaliza miongoni mwa Nne Bora EPL na kupata tiketi ya kufuzu kwa michuano ya Klabu Bingwa Ulaya.

“Tumerejea vyema na kupata ushindi ambao umetuwezesha kubakia na matumaini ya kushiriki mechi za Klabu Bingwa,” aliongeza Kane ambaye alicheza licha ya kuwa na maumivu ya ghafla.

“Tulikuwa na mazungmzo miongoni mwetu, na matokeo yameanza kuonekana. Wachezaji walizungumza wazi na safari imeanza vizuri. Kwa hakika yalikuwa mazungumzo muhimu baada ya kusuasua katika mechi kadhaa za karibuni.”

“Tumedhihirisha kwamba umoja ni nguvu. Tulimhakikishia kocha ushindi ambao tumempa na tungependa kuendelea hivyo,” aliongeza nahodha huyo mwenye umri wa miaka 29.

Hata hivyo, Fulham watajilaumu kwa kupoteza nafasi nyingi walizopata kwenye mechi hiyo, kabla ya Kane kumimina wavuni bao la ushindi dakika ya 45, ambalo limekiwezesha kikosi hicho cha Antonio Konte kushikilia nafasi ya tano jedwalini.

Bao la Kane lilikuwa la 199 ligini kwa mshambuliaji ambaye ameichezea klabu hiyo mara 300, wakati akikaribia kuvunja rekodi ya Greaves ya miaka 53.

Spurs wamekuwa wakilemewa katika mechi za karibuni, huku kipa wao Hugo Lloris akionekana kushuka kiwango.

  • Tags

You can share this post!

MITAMBO: Mtambo safi katika uundaji lishe toka makapi ya...

Yeye hugeuza uchafu kuwa sanaa inayolipa

T L