Mkutano wa kilele wa Jumuiya ya Madola waanza nchini Rwanda

Mkutano wa kilele wa Jumuiya ya Madola waanza nchini Rwanda

NA MASHIRIKA

KIGALI, RWANDA

MARAIS na mawaziri wakuu kutoka mataifa mbalimbali ulimwenguni Ijumaa Juni 24, 2022 wameanza mkutano wa kilele wa Viongozi wa Mataifa wanachama wa Jumuiya ya Madola (CHOGM) jijini Kigali, Rwanda.

Waziri Mkuu wa Uingereza Boris Johnson aliwasili nchini humo Alhamisi na kufanya mkutano na Rais wa Rwanda Paul Kagame.

“Walijadili mikataba mbalimbali ya ushirikiano kati ya Rwanda na Uingereza, ikiwemo ushirikiano kuhusu Uhamiaji na Ustawi wa Kiuchumi,” ikulu ya Rwanda ilisema kupitia twitter.

Mkataba kuhusu mpango wa kuwapa makao wahamiaji umekumbwa na pingamizi ikiwemo vikwazo vya kisheria.

Viongozi wengine kutoka mataifa 54 wanachama wa jumuiya hiyo waliendelea kuwasili jijini Kigali jana kwa mkutano huo unaoanza Jumatatu.

Mengi ya mataifa hayo ni yale ambayo yalikuwa chini ya Ukoloni wa Uingereza.

Rwanda ilikuwa koloni ya mataifa ya Ujerumani na Ubelgiji lakini ilijinga na jumuiya ya Madola mnamo 2009.

Kufikia jana, zaidi ya viongozi 25 wa serikali walikuwa wamesili jijini Kigali, miongoni mwao wakiwa ni; Rais wa Nigeria Muhammadu Buhari, Waziri Mkuu wa Canada Justin Trudeau, Yoweri Museveni wa Uganda na Rais wa Kenya Uhuru Kenya.

Mwanamfalme Charles – anayewakilisha mamake, Malkia Elizabeth – na mkewe Camilla, waliwasili Rwanda mnamo Jumanne.

Wanandoa hao walizuru eneo la Kumbumbuku ya Mauaji ya Halaiki jiji Kigali ambako waliweka shada la maua na kuhudhuria ibada kanisani.

Aidha, walikutana na manusura wa mauaji hayo yalitokea mnamo 1994 katika kijiji kimoja kilichoko Mashariki mwa Rwanda.

Mwanamfalme Charles na Camilla pia walikutana na Rais Kagame na Rais Museveni.

Rais Museveni alifika Rwanda kupitia eneo la mpaka la Gatuna/Katuna.

Mpaka huo ulikuwa umefungwa kwa muda wa miaka mitano kufuatia uhusiano mbaya kati ya Uganda na Rwanda.

Viongozi wa mataifa wanachama wa Jumuiya ya Madola watajadili masuala mbalimbali yenye umuhimu kwa jumuiya hiyo kando na kutoa hotuba rasmi.

Waziri Mkuu Trudeau pia atafungua rasmi ubalozi wa Canada jijini Kigali.

TAFSIRI NA: CHARLES WASONGA

  • Tags

You can share this post!

Hoki: Mechi 3 kupigwa Jumapili

KIKOLEZO: Kali za 254 Netflix

T L