Habari Mseto

Mkutano wa Munya wazua uhasama wa madiwani

June 13th, 2020 1 min read

NA DAVID MUCHUI

Mkutano ulioitishwa na Waziri wa Kilimo Peter Munya Jumamosi nyumbani kwake umefufua vita vya kisiasa kati ya waziri huyo na Gavana Kiraitu Murungi .

Madiwani wanaoegemea upande wa Bw Munya walimlaumu kiongozi wa wengi katika bunge la kaunti hiyo ya Meru Victor Karithi kwa kuwachochea madiwani wa chama cha wa Jubilee wasihudhurie mkutano huo.

Kiongozi wa wachache Ayub Bundi na diwani mteule Sarah Gakii walisema kwamba Bw Karithi anafaa kulaumiwa kwa kuharibu mkutano huo.

Bi Gakii alisema kwamba mkutano huo utajadiliana kuhusu miradi ya maendeleo na marekebisho ya wakulima wa Meru.

“Bw Munya ameitisha mkutano ili kusikiza mambo yanayowathiri wakulima. Sielewi ni kwa nini kiongozi wa wengi anawaonya madiwani wa Jubilee kutohudhuria,” Bi Gakii alisema.

Bi Gakii aliongeza kwamba madiwani wa chama cha Jubilee walionywa kwamba watachukuliwa hatua kali wakihudhuria mkutano huo.

Alisema kwa Bw Murithi alikuwa amepewa maelezo hayo ya kuharibu mkutano huo na Gavana Kiraitu.

“Inasitikisha kuona kiongozi wa wengi akiwaagiza madiwani wasihudhurie mkutano wa maendeleo kwa manufaa ya binafsi.

“Wananchi wanapaswa kujua kwamba madiwani ambao hawatahudhuria mkutano huo hawatakii wananchi mazuri.Wapaswa kuhudhuria mkutano huo iliwapeane maoni ya nini wanachi wanataka kufanyike katika skta ya ukulima,alisema..

Bw Murithi alisema kwamba hakuwa ameangizwa na kiongozi yeyote kuhudhueria mkutano wowote.

“Kiongozi yeyote ako huru kuweka mkutano na madiwani ,wabunge na viongozi wengine bora wazingatie mikakati iliyowekwa ili kudhibiti kusambaa kwa corona,” alisema Bw Karithi.