Mkuu wa zamani NHIF aondolewa kesi ya Sh1.1b

Mkuu wa zamani NHIF aondolewa kesi ya Sh1.1b

Akitamatisha kesi dhidi Bw Mwangi , hakimu mkuu Victor Wakumile alimshauri Haji atathmini upya kesi dhidi ya washtakiwa wenza 17 wa kinara huyo wa zamani wa NHIF.

Kuachiliwa kwa Bw Mwangi kumetokea wiki mbili baada ya kuachiliwa kwa mwenyekiti wa mamlaka ya mawasiliano (CA) Mary Wambui aliyeshtakiwa kwa kukataa kulipa ushuru wa Sh2.2bilioni.

Kabla ya kutamatishwa kwa kesi dhidi ya Wambui kulitekelezwa baada ya kesi dhidi ya Mawaziri Aisha Jumwa na Mithika Linturi.

Akitamatisha kesi dhidi ya Bw Mwangi hakimu alisema DPP amedokeza hakuna pesa zilizopotea na kwamba tenda ya kuidhinisha ukusanyaji wa ada za bima ya NHIF utekelezwe kimitandao uliidhinishwa na bodi yote ya NHIF na kwa mujibu wa sheria.

Bw Mwangi alishtakiwa pamoja na aliyekuwa kinara wa NHIF Simeon Kirgotty na wanachama wa kamati ya ukaguzi iliyowajumuisha Mudzo Nzili, Yussuf Ibrahim na Elly Nyaim.

Wengine walioshtakiwa ni Ruth Sidoi, Gilbert Gathuo, Irene Rono, Yusuf Ibrahim, Joseph Mbuvi, Pamela Marendi, Gibson Muhuhu, Jacinta Mwangi, Kennedy Wakhu, Fredrick Onyancha, Millicent Mwangi na Darius Philip Mbogo.

  • Tags

You can share this post!

Sambakhalu FC watwaa Lwanga Cup

Jambazi ‘msaliti’ aomba atumikie kifungo cha nje

T L