Kimataifa

Mlipuko wa bomu garini wasababisha vifo vya zaidi ya watu 70 Mogadishu

December 28th, 2019 1 min read

Na MASHIRIKA

WATU zaidi ya 70 wamefariki katika shambulio la bomu katika gari lililotekelezwa Jumamosi asubuhi jijini Mogadishu, Somalia, amesema mkuu wa hospitali ya Medina, Mohamed Yusuf akizungumza na mashirika ya habari.

Yusuf amesema takribani majeruhi 54 wamefikishwa katika hospitali hiyo kupata huduma za kimatibabu.

Idadi jumla ya walioangamia inakadiriwa kuwa 76 huku waliojeruhiwa wakiwa ni watu 70.

Walioshuhudia tukio hilo wameelezea taswira ya hali ya majonzi eneo la mkasa mara baada ya gari lililokuwa eneo la ukaguzi kulipuka katika eneo la jiji lenye utitiri wa shuguli.

Kufikia sasa hakuna kundi lolote lililokiri kuhusika na shambulio hilo.