Mlipuko wa ugonjwa wa kuhara wazua hofu vijijini Boni

Mlipuko wa ugonjwa wa kuhara wazua hofu vijijini Boni

Na KALUME KAZUNGU

MLIPUKO wa maradhi ya kuendesha na kutapika umeibuka miongoni mwa watoto kwenye vijiji vya msitu wa Boni, Kaunti ya Lamu.

Takriban watoto 200 wameripotiwa kuugua maradhi hayo yanayokisiwa kuchangiwa na matumizi ya maji machafu katika vijiji vya Kiangwe, Mangai, Milimani na Basuba.

Waziri wa Afya katika Kaunti ya Lamu, Bi Anne Gathoni, alithibitisha maradhi hayo ya lakini akasema idara yake tayari imedhibiti hali hiyo.

“Ni kweli. Kumekuwa na visa vya kuharisha na kutapika miongoni mwa watoto eneo la Msitu wa Boni. Tunaendelea kuidhibiti hali hiyo,” akasema Bi Gathoni.

Diwani wa Wadi ya Basuba, Barissa Deko aliiomba serikali ya kaunti ya Lamu kufanya mpango wa haraka kupeleka wahudumu wa afya eneo hilo ili kusaidia kuwatibu wakazi, hasa watoto ambao ndio walioathirika zaidi

Bw Deko pia aliisisitizia idara ya afya ya umma kusambazia wakazi dawa za kusafisha maji eneo hilo.

“Tunaomba madaktari waletwe hapa. Pia wasambaze dawa za kutibu maji vijijini ili kizuia mlipuko zaidi wa maradhi,” akasema Bw Deko.

You can share this post!

KAMAU: Tamaa imegeuza Afrika kuwa ‘soko la utumwa’

Vigogo wa KNUT, KUPPET sasa waanza kuhemeshwa