Habari Mseto

Mlipuko watokea Mogadishu

July 4th, 2020 1 min read

ABDULKADIR KHALIF

Mlipuko mkubwa ulisikika kwenye mji mkuu wa Somalia Mogadishu mapema Jumamosi.

Ripoti zilisema kwamba mnamo saa moja na nusu asubuhi kuna gari liliangukia ukuta karibu na bandari na likalipuka.

Maelezo yalikuwa machache huku maafisa wa wakushughulikia dharura wakishughulikia hali hiyo, lakini polisi walisema kwamba watapeana habari zaidi baadaye.

Kufikia sasa hakuna kikundi kilichojitokeza na kudai kuhusika na mlipuko huo wa asubuhi.

Wafanyavibarua wengi hutembea bandarini asubuhi na mapema kutafuta kazi.