Mmiliki wa Hoteli kukamatwa kwa ulaghai wa Sh.520Milioni

Mmiliki wa Hoteli kukamatwa kwa ulaghai wa Sh.520Milioni

Na RICHARD MUNGUTI

MMILIKI wa msururu wa mahoteli ya Nyamama yaliyoko kaunti ya Nairobi jana aliagizwa akamatwe na kushtakiwa kwa ulaghai wa  benki Sh520milioni.

Idara ya Uchunguzi wa Jinai (DCI) iliagizwa Jumatano imtie nguvuni Bi Nina Jayesh Shanghavi na kumfikisha mahakamani Desemba 14, 2021 kujibu shtaka la kuilagahi Victoria Commercial Bank Limited kati ya 2018 na 2020.. Nina anayeshtakiwa pamoja na mumewe Jayesh Umedlal Shanghavi alisemekana amesafiri ng’ambo.

Wakili Edwin Salun aliomba mahakama isitishe kibali cha kumkamata Nina kwa vile yuko ng’ambo.Salun anamtetea Jayesh na mkewe Nina. Salun anayemtetea Nina alimweleza hakimu mwandamizi Wandia Nyamu alimfahamisha afisa anayechunguza kesi hiyo aliko mshtakiwa huyo na kuomba korti ifutilie mbali agizo la kumkamata hadi atakaporudi  kutoka ng’ambo kabla ya aidha Desemba 22, 2021 ama mbeleni.

Mahakama ilifahamishwa maafisa kutoka afisi ya DCI walipofika katika makazi yao washtakiwa walipata Nina ameondoka kwenda ng’ambo. “Polisi walifika katika makazi yao washtakiwa na kupata Nina amesafiri,”Salun alisema Wakili huyo aliomba mahakama isitishe kibali cha kumtia nguvuni ilichokitoa wiki mbili zilizopita.

“Noamba hii mahakama imruhusu mshtakiwa afike kortini Desemba 22 kujibu mashtaka yanayowakabili na mumewe Jayesh Umedlal Shanghavi ya ulaghai wa Sh520milioni,” hakimu aliombwa na wakili wa washtakiwa hao. Bi Nyamu alimkubalia Nina kufika kortini Desemba 22, 2021 atakapojibu shtaka.

Hakimu alisema endapo mshtakiwa atarudi mapema kutoka ng’ambo anaweza kufika kortini kusomewa mashtaka. Nina na Jayesh wanakabiliwa na shtaka la kupokea pesa Sh520milioni kutoka benki ya Victoria Commercial Bank kati ya  Desemba 10 2018 na Aprili 23 2020.

Wawili wanadaiwa walitumia hati za umiliki wa ardhi ambapo nyumba za kampuni ya Crystal Edge Apartment. Na wakati huo huo mahakama ilikataa kumruhusu Jayesh asafiri kwenda Dubai kuanzia  Desemba 9,2021. Upande wa mashtaka ulipinga mshtakiwa akisafiri ukisema “Jayesh na Nina hawawezi kuruhusiwa kuwa nje wote.”

Mahakama iliamuru Jayesh arudi kortini Desemba 14 kupokea uamuzi ikiwa ataruhusiwa kusafiri au la.

 

You can share this post!

Jaji Said Juma Chitebwe ashtaki JSC kuhusu video zake na...

‘Straika’ Mbrazil aliyeshindwa kupepetea K’ Ogalo

T L