Montreal anayochezea Wanyama yaona cha mtema kuni dhidi ya LA Galaxy

Montreal anayochezea Wanyama yaona cha mtema kuni dhidi ya LA Galaxy

Na GEOFFREY ANENE

CF Montreal imenyolewa bila maji 4-0 mikononi mwa Los Angeles Galaxy kwenye Ligi Kuu ya Amerika na Canada (MLS) ugani Carson, Jumanne.

Montreal, ambayo imeajiri kiungo Mkenya Victor Wanyama, iliongoza kipindi cha kwanza 2-0 kupitia mabao ya Javier “Chicharito” Hernandez dakika ya nane na penalti ya Dejan Joveljic dakika ya nne nyongeza.

Rayan Raveloson aliimarisha uongozi wa LA Galaxy hadi 3-0 dakika ya 59 kabla ya kuhitimisha dakika ya 79.

Montreal ya kocha Wilfried Nancy ilitawala mchuano huo ikiwemo katika upigaji wa kona 7-4 na umilikaji wa mpira 62-38, lakini wenyeji LA Galaxy walikuwa na shabaha zaidi.

Ni kichapo cha nne mfululizo cha Montreal dhidi ya LA Galaxy baada ya 2-0 Aprili 2017, 1-0 Mei 2018 na 2-1 Septemba 2019.

Montreal sasa ni nambari tatu katika ligi ya MLS ya ukanda wa mashariki nyuma ya New York Red Bulls na Philadelphia Union nayo LA Galaxy inakamata nafasi ya nne kwenye ukanda wa magharibi nyuma ya Los Angeles FC, Austin FC na Real Sal Lake.

  • Tags

You can share this post!

Barcelona yasajili vigogo Franck Kessie na Andreas...

Kibarua ashtakiwa kwa kuvunja vioo vya madirisha ya kituo...

T L