Montreal yapiga hatua ya kuingia Klabu Bingwa CONCACAF kwa kulima Forge nchini Canada

Montreal yapiga hatua ya kuingia Klabu Bingwa CONCACAF kwa kulima Forge nchini Canada

Na GEOFFREY ANENE

CF Montreal anayochezea Victor Wanyama imeweka hai matumaini ya kuingia Klabu Bingwa Amerika Kaskazini, Kati na Carribean (CONCACAF) mwaka 2023 kupitia mashindano ya Canada baada ya kubwaga Forge 3-0 ugani Saputo, Alhamisi.

Vijana wa kocha Wilfried Nancy walipata mabao yao yote kupitia kwa mshambulizi wa Nigeria, Sunusi Ibrahim katika dakika ya 14, 22 na 49.

Kiungo mkabaji Wanyama, ambaye ni mmoja wa manahodha wa Montreal, hakuwa kikosini. Montreal ni mabingwa watetezi wa kipute hicho cha Canada. Walishiriki Klabu Bingwa ya CONCACAF mwaka huu kwa sababu ya kutawala kipute cha Canada mwaka 2021, lakini wakabanduliwa mapema.

Walilemea Santos Laguna kutoka Mexico katika raundi ya 16-bora kwa jumla ya mabao 3-1 Februari kabla ya kupigwa na Cruz Azul kutoka Mexico kwa jumla ya mabao 2-1 Machi katika robo-fainali.

Kujikatia tiketi ya Klabu Bingwa msimu ujao lazima Montreal wapepete wenzao kutoka Ligi Kuu ya Amerika na Canada (MLS) Toronto katika nusu-fainali Juni 20 na mshindi kati ya Vancouver Whitecaps na York United, katika fainali.

Wanyama, ambaye kandarasi yake ya miaka mitatu kambini mwa Montreal itakatika Desemba 31, 2022, amecheza jumla ya mechi 68 zikiwemo 16 msimu huu.

  • Tags

You can share this post!

Mohamed Salah asema atasalia Liverpool msimu ujao

Hakuna kama Jose!

T L