Moraa na Korir mawindoni Stockholm Diamond League kinyume na ombi la AK

Moraa na Korir mawindoni Stockholm Diamond League kinyume na ombi la AK

Na GEOFFREY ANENE

WAKENYA Mary Moraa na Emmanuel Korir watatimka mbio za mita 800 kwenye duru ya nane ya Diamond League jijini Stockholm, Uswidi, leo Alhamisi jioni.

Hiyo ni licha ya Shirikisho la Riadha Kenya (AK) kuonya wanariadha walio kambini uwanjani Kasarani kwa ajili ya Riadha za Dunia, wasishiriki mashindano mengine.

Moraa, ambaye alijikatia tiketi ya Riadha za Dunia mnamo Juni 24-25 ugani Kasarani, atakabiliana na wakimbiaji matata wakiwemo mshindi wa Kip Keino Classic Prudence Sekgodiso (Afrika Kusini), bingwa wa dunia Halimah Naakayi (Uganda) na mshindi wa nishani ya fedha ya Olimpiki, Keely Hodgkinson (Uingereza).

Mfalme wa Olimpiki Korir atapimana ubabe na Wakenya wenzake Collins Kipruto na Ferguson Rotich, bingwa mpya wa Afrika Slimane Moula (Algeria) na Mfaransa Benjamin Robert miongoni mwa wengine.

Korir alishinda misimu ya Diamond League 2018 na 2021. Rotich atatetea taji la Stockholm.

Virginia Nyambura, Fancy Cherono na Rosefline Chepng’etich watatimka katika mbio za mita 3,000 kuruka viunzi na maji, Boaz Kiprugut na Cornelius Kemboi katika mita 3,000.

  • Tags

You can share this post!

TAHARIRI: IEBC isikubali presha za mirengo, ifuate sheria

Gikaria, Arama, Ngunjiri wahojiwa kuhusu genge la...

T L