Morata afunga mabao mawili na kusaidia Juventus kuangusha Lazio kwenye Serie A

Morata afunga mabao mawili na kusaidia Juventus kuangusha Lazio kwenye Serie A

Na MASHIRIKA

MSHAMBULIAJI Alvaro Morata alifunga mabao mawili na kusaidia Juventus kutoka nyuma na kusajili ushindi wa 3-1 dhidi ya Lazio kwenye mechi ya Ligi Kuu ya Italia (Serie A) mnamo Jumamosi usiku.

Cristiano Ronaldo alisazwa kwenye benchi na nafasi yake kutwaliwa na Morata anayewachezea Juventus kwa mkopo kutoka Atletico Madrid ya Uhispania.

 Joaquin Correa aliwaweka Lazio uongozini katika dakika ya 14 kabla ya juhudi zake kufutwa na Adrien Rabiot aliyesawazisha mambo kunako dakika ya 39.

Morata alicheka na nyavu za Lazio katika dakika ya 57, sekunde chache kabla ya kufunga penalti iliyokuwa zao la Sergej Milinkovic-Savic kumchezea visivyo kiungo wa zamani wa Arsenal, Aaron Ramsey.

Ushindi kwa Juventus ya kocha Andrea Pirlo uliwadumisha katika nafasi ya tatu jedwalini kwa alama 52, saba nyuma ya viongozi Inter Milan wanaonolewa na kocha wa zamani wa Chelsea, Antonio Conte. AC Milan wanakamata nafasi ya tatu kwa pointi 53, nne mbele ya Atalanta wanaofunga mduara wa nne-bora.

MATOKEO YA SERIE A (Machi 6, 2021):

Juventus 3-1 Lazio

Spezia 1-1 Benevento

Udinese 2-0 Sassuolo

TAFSIRI NA: CHRIS ADUNGO

  • Tags

You can share this post!

Leicester City wacharaza Brighton na kutua nafasi ya pili...

Chipukizi Moriba asaidia Barcelona kuziba pengo la alama...