Michezo

Motisha ya mashabiki nguzo ya Kibra United

February 4th, 2020 2 min read

Na JOHN KIMWERE

KIBRA United na Gogo Boys zote kutoka Kibera, Nairobi zinajisuka upya kwenye mechi za Kundi A Ligi ya Taifa Daraja la Pili msimu huu.

Kibra ya kocha, Kelvin Aringa iliyoibuka ya kumi muhula uliyopita inalenga kufanya yake. Mashemeji hao wameibuka kati ya timu tano zinazotifua vumbi la kufa mtu kwenye kampeni za msimu huu.

”Bila kujipigia debe muhula huu wafuasi wetu wamewapa wachezaji motisha zaidi ambapo tumepania kumaliza kileleni na kujiweka pazuri kutwaa tiketi ya kupandishwa ngazi,” anasema meneja wa Kibra United, Saidi Rajabu na kudai kusokawa wachezaji wake tayari wamejipatia ubingwa mapema.

Timu ya Butterfly FC maarufu King of Ruiru. Picha/ John Kimwere

Kibra United chini ya nahodha, Nassor ‘Alolo’ Yusuf inajikaza kiume kweli ambapo bada ya kusakata mechi 11 maana imeshinda mara saba na kutoka nguvu sawa mara moja na kupoteza patashika moja.

Kibera baada ya kushuka dimbani mara 11 wametua kileleni kwa alama 23 sawa na Ruiru Hotstars inbayokuja kiana kwenye kampeni za muhula huu.

Kiasi Kibra United, Ruiru Hotstars na Gogo Boys zimepata afueni maana wapinzani wengine, Butterfly maarufu King of Ruiru wamepata pigo kwa kupokonywa alama sita muhimu kwa kuvamia mwamuzi wa mechi hizo.

Kibra inazidi kufanya vizuri kutokana na juhudi za wanyakaji wake Edward Apuk, Malik Omondi na Moses Ndambuki.

Baadhi ya wachezaji wa timu ya Hospitali ya Kitaifa ya Kenyatta (KNH) inayoshiriki kipute hicho. Picha/ John Kimwere

Meneja huyo anadokeza kuwa kikosi hicho kinajumuisha wachezaji wazoefu ambapo wakizidi kumanika bila watabeba taji hilo.

”Nina kikosi kinaoonekana kimeiva vizuri kuvuruga wapinzani wengine na kufanya kweli,” alisema na kusema wafuasi wao wamewapa motisha zaidi kwa kuzingatia wanawafuata kwa kila mechi wanaoshiriki ya ngarambe hiyo.

Naye mwenyekiti wa Gogo Boys, Abdul Suleiman inayofunga tatu bora kwa alama 18 anasema “Kampeni za kipute cha msimu huu kinazidi kuzua msisimko mkali hasa baina yetu na mashemeji wetu Kibra United.”

Baadhi ya wachezaji wa South B Allstars inayoshiriki ngarambe hiyo. Picha/ John Kimwere

Ofisa huyo anasisitiza kuwa huenda mechi ndizo zitakaoamua mabingwa wa kinyang’anyiro hicho. Gogo Boys chini ya nahodha, Yusuf Ali ina mchezo mmoja kapuni ambapo bado imekaa pazuri kuwapiga mashemeji wao.

Anadai licha ya pengo lililo kati ya vikosi hivyo kamwe hawana shaka wanaamini wanatosha kukaza buti na kuteka ubingwa wa mashindano ya msimu huu.

Gogo Boys inategemea kati ya wachezaji ambao wameibuka kaa la moto wakishuka dimbani wakiongozwa na nahodha huyo, Yusuf Ali, Khubeib Ali, Hillary Shirao kati ya wafungaji hatari sio haba, Kelvin Senya, Gilbert Omondi na Collins Idapa.