Habari

Moto usiku wasababisha taharuki Mombasa Hospital

November 12th, 2019 1 min read

Na MISHI GONGO

TAHARUKI imetanda Jumanne usiku katika Mombasa Hospital – ya mmiliki binafsi – baada ya moto kuteketeza jengo moja katika hospitali hiyo.

Kamishna katika Kaunti ya Mombasa Bw Gilbert Kitio akithibitisha kutokea kwa mkasa huo amesema moto huo ulianza mwendo wa saa tatu usiku katika eneo la jikoni kabla ya kusambaa.

Zimamoto kutoka kaunti hiyo wamekuwa wakifanya kulihali kujaribu kudhibiti moto huo ili usienee.

Muda wa saa moja baadaye, moto huo ulikuwa haujazimwa kabisa.

Bw Kitio ameeleza kuwa hakuna aliyejeruhiwa japo baadhi ya wagonjwa, ilibidi wahamishwe na kupelekwa hospitali jirani kwa usalama.

Walio katika eneo la mkasa ambao wamesema sehemu zilizoathirika zaidi ni chumba cha wagonjwa mahututi, wodi ya uzazi na baadhi ya wodi nyinginezo.

Jumatatu hospitali kuu ya Pwani ya Makadara palitokea moto hapo, lakini haukuwa mkubwa na ulizimwa upesi.

 

Tunafuatilia mkasa huo na tutaendelea kutoa maelezo zaidi…