Habari Mseto

Moto wasababishia wakazi hasara ya Sh50m

June 29th, 2020 1 min read

NA RUTH MBULA NA FAUSTINE NGILA

Wakulima wa kikundi cha Keyian kaunti ya Transmara Magharibi wanakadiria harasa ya Sh50 milioni baada ya moto kuteketeza shamba lao la miwa Jumamosi.

Mwenyekiti wa kikundi hicho Bw Phillip Saiyuah alisema kwamba hekari 200 za mashamba yao ziliharibiwa na moto.

Bw Saiyuah alisema kwamba moto huo ulianzishwa na mtu asiyejulikana usiku na nia yake haijulikani.

“Tumepata hasara kubwa sana. Tunaomba serikali kufanya uchunguzi ili kubaini chanzo cha moto huo na wanaohusika wachukuliwe hatua,”alisema B Saiyuah.

Alisema kwamba miwa hiyo ilikuwa imekomaa tarayi kuvunwa.

“Mashamba yetu yanapatikana kwenye mpaka wa Kisii na Masaai na ni vizuri jambo hilo lishungulikiwe  na mamlaka ili kuepuka mizozo ya mipakani,” alisema mwenyekiti wa kikundi hicho.

Meneja wa mashamba hayo David Kuya  alisema kwamba kuchomwa kwa miwa ilokiomaa ni kulemaza uchumi chini.

 “Ni uchungu sana kwasababu mamia ya watu hutengemea mashamba hayo kukidhi maitaji yao.Kusababisha harasa kama hio wakati huu wa corona ni janga mara mbili,” alisema Bw Momposhi.