Kimataifa

Moto wateketeza gereza kuu la Kondengui nchini Cameroon

July 23rd, 2019 1 min read

Na MASHIRIKA

YAOUNDE, CAMEROON

MOTO mkubwa ulizuka Jumatatu katika gereza kuu la Kondengui jijini Yaoundé nchini Cameroon wakati wafungwa wengi wanaoaminika kutokea katika maeneo yanayozungumza Kiingereza kuandamana wakishinikiza waachiliwe.

Milio ya risasi pia ilisikika katika gereza hilo.

Msemaji wa chama cha upinzani, Social Democratic Front (SDF), amesema wafungwa wanne waliuawa na wengine kadhaa kujeruhiwa wakati risasi za moto zilitumika na vilevile mabomu ya kutoa machozi.