Moto waua watu wanne katika soko la Toi jijini Nairobi
WATU wanne walifariki alfajiri ya Jumamosi ya Agosti 3, 2024 katika soko la Toi liliko Kibera, Kaunti ya Nairobi, kutokana na moto ambao uliwaacha wafanyabiashara wakikadiria hasara tele.
Chifu wa eneo la Woodley, Nehemia Amwocha, alisema watu wanne walioangamia walikuwa wakijaribu kuokoa bidhaa zao.
“Moto huo ulianza dakika mbili kabla ya saa kumi asubuhi. Kuna watu watatu na mtoto mmoja ambao walifika hapa kuokoa mali yao. Moto huo uliwazidi na wakapoteza maisha,” alisema Bw Amwocha.
Miili ya wanne hao ilipelekwa katika hifadhi ya maiti ya City jijini Nairobi.