Habari Mseto

Motoni kwa kumng'oa meno mkewe

September 1st, 2020 1 min read

Na Joseph Ndunda

Mwanaume aliyemtesa mkewe na kumng’oa meno mawili ameshtakiwa kortini kwa kumsababishia majeraha mabaya.

Felix Ochieng Owino alishtakiwa kwa kusababisha majeraha kwa Ruth Anyina nyumbani kwao Silanga, Kibera.

BI Anyona alikuwa amerudi akitoka kuwatembelea wazazi wake alipopata mume wake na kumwambia kwamba wazazi wake walikuwa wanahitaji usaidizi .

Hapo ndipo mumewe alichukua kijiti alichotumia kumpiga. Alipata majerahaa kifuani, jicho la upande wa kushoto na mdomoni.

Polisi walipata meno hayo mawili yaliyotumika kama ushahidi. Bw Owino alikana mashtaka hayo alipofika mbele ya  hakimu mkuu Philip Mutua kwenye korti ya Kibera.

Aliachiliwa kwa dhamana ya 500,000. Kesi hiyo itasikizwa tena Septemba 16.

Tafsiri na Faustine Ngila