Habari Mseto

Motono kwa kujaribu kuiba mamilioni ya Equity

August 18th, 2020 1 min read

Na RICHARD MUNGUTI

MWANAUME alishtakiwa kujaribu kuibia benki ya Equity Sh18m.

Justus Mutinda Ndolo alikana mashtaka matatu ya kujaribu kuibia benki hiyo , wizi wa Sh314,774 na kupatikana na pesa zilizodhaniwa zimeibwa katika akaunti yake iliyoko kwenye benki hiyo ya Equity.

Ndolo aliyefikishwa mbele ya hakimu mwandamizi Bernard Ochoi alikana mashtaka dhidi yake na kuomba aachiliwe kwa dhamana.

Mshtakiwa alipewa dhamana ya Sh500,000 pesa tasilimu.

Mashtaka ni kwamba kati ya Mei 8 na Agosti 12,2020 alijaribu kuibia benki ya Equity $172,445 sawa na Sh18,969,968.

Kesi itatajwa mnamo Agosti 31 2020.