Habari Mseto

Mount hachoki kupenda, kajinasia banati mwenye umbo la tausi!

April 27th, 2024 1 min read

NA CHRIS ADUNGO

MASON Mount amezua tetesi mpya za mahaba baada ya kunaswa na kamera akisisimuana na kidosho ambaye bado hajatambuliwa jina.

Fowadi huyo wa Manchester United alifurahia mapumziko yake majuzi kwa kuvinjari eneo la Altrincham viungani mwa jiji la Manchester, Uingereza.

Mason, 25, alionekana akitembea na mrembo wakielekea kwa gari lake aina ya Land Rover Defender 4×4 lililomgharimu Sh20 milioni majuzi.

Mchezaji huyo wa zamani wa Chelsea anapata hifadhi mpya ya penzi lake kwa mrembo huyo, miaka miwili baada ya kutemana na kipusa Chloe Wealleans-Watts aliyekula naye bata kwa kipindi cha miaka mitano kuanzia Desemba 2017.

Baada ya kubwagana na Chloe – mzawa wa mji wa Portsmouth nchini Uingereza – Mason wakati huo alisema kikubwa alichopania kufanya ni “kujikuza zaidi katika soka.”

Sogora huyo amewahi pia kuburudishwa na mwanamitindo Astrid Wett ambaye aliwahi vile vile kuhusishwa na wanasoka Saido Berahino na Marouane Fellaini.

Kabla kuanza kuchovya asali ya Astrid mnamo 2021, Mount alikuwa akitoka na kidosho Orla Sloan almaarufu ‘Devil Baby’.

Tunda la kichuna huyo liliwahi pia kudokolewa na wachezaji Billy Gilmour wa Brighton na Ben Chilwell wa Chelsea.

Mount amekosa mechi mbili zilizopita za Man-United kutokana na jeraha. Alikosa kuunga kikosi kilichodengua Coventry kwenye nusu-fainali ya Kombe la FA na kile kilichokomoa Sheffield United 4-2 katika Ligi Kuu ya Uingereza (EPL), Jumatano.

Sogora huyo amewahi pia kuburudishwa kimapenzi na mwanamitindo Astrid Wett aliwahi vilevile kuhusishwa na wanasoka Saido Berahino na Marouane Fellaini.

Kabla ya kuanza kuchovya asali ya Astrid mnamo 2021, Mount alikuwa akitoka kimapenzi na kidosho Orla Sloan almaarufu ‘Devil Baby’.

Tunda la kichuna huyo liliwahi pia kudokolewa na wachezaji Billy Gilmour wa Brighton na Ben Chilwell wa Chelsea.