Habari Mseto

Mpango wa kumng'oa Obado waanza

August 30th, 2020 1 min read

Na Justus Ochieng’

MASAIBU yanazidi kumwandama Gavana  wa Kaunti ya Migori Okoth Obado huku ripoti zikisema kwamba kuna mpango wa mswada wa kumng’oa mamalakani kufuatia mashtaka yake ya utumizi mbaya wa mamlaka.

Siku yenye korti ilimzuia Obado kuingia afisini mwake, chama cha ODM kiliwaita madiwani wake mkutano huku nduru za kuamikina zikisema kwamba kuna uwezekano wa kuwa wanalizungumzia mswada wa kumng’oa mamlakani Bw Obado.

Jumatatu hakimu mkuu Lawrence Mugambi wa korti ya Milimani alimwachilia Obado kwa dhamana ya Sh8.7 milioni na kumzuia kusafiri nje ya nchi.

Kufuatia hayo chama cha ODM ambacho kinawatu wengine kweenye bunge hilo la Migori kiliwaita wanachama wake kwenye, mkutano wa ushari”Nairobi Leo.

Mkurugenzi mtendaji  wa chama cha ODM aliandikia  mkubwa wa wengi wa bunge hilo la Migori Keke Oyugi Jumatatu akimwomba kuwaalika madiwani wengine kwenye mkutano.

Tafsiri na Faustine Ngila