Habari Mseto

Mpenzi wa zamani wa Ruben Dias amtema kiungo wa Sheffield kama chingamu

April 13th, 2024 2 min read

NA CHRIS ADUNGO

KIUNGO mkabaji wa Sheffield United na timu ya taifa ya Brazil, Vinicius de Souza Costa, ameachwa kwa mataa baada ya mwigizaji maarufu wa Uingereza, Arabella Chi, kumtema kama chingamu.

Sogora huyo, 24, alianza kumtambalia Arabella, 33, kimapenzi mwezi jana; wiki chache baada ya kisura huyo kutemana na mwigizaji na mwanamiereka mahiri wa Northern Ireland, Adam Maxted.

Awali, tunda la kichuna huyo lilikuwa likidokolewa na beki mzoefu wa Manchester City na timu ya taifa ya Ureno, Ruben Dias.

De Souza alipigwa na butwaa Jumanne alipotambua Arabella amejisajili kwa programu ya Raya, inayotumiwa na watu maarufu kutafuta wapenzi wapya mitandaoni.

Aidha, demu huyo alimpiga bloku kwenye mitandao yote ya kijamii huku akifuta pia kwenye Instagram picha zote walizokuwa wamepigwa pamoja wakiwa kwenye ziara mbalimbali za burudani.

Kwa mujibu wa gazeti la The Sun, Arabella amekuwa akibadilishana jumbe za kimapenzi na wanaume kadhaa kupitia programu ya Raya ila tahadhari kubwa anayoichukua ni kutohusiana tena kimapenzi na mwanasoka.

Arabella alivyobwagana na De Souza

Japo haijulikana ni lini hasa ambapo Arabella alibwagana na De Souza, uhusiano wa kipusa huyo na Dias, 26, pia ulivunjika ghafla mwanzoni mwa mwaka huu baada ya kuchumbiana kwa muda mfupi kuanzia Septemba 2023.

Alipata hifadhi mpya ya penzi lake kwa Maxted kabla ya kuanza kutambaliwa na De Souza muda mfupi baadaye.

“Amekuwa akifuatiliwa na madume kadhaa tangu apakie picha na video zake nusu uchi. Ingawa idadi kubwa ya wanaume wanaomvizia ni wanasoka, ni kama hana mpango wa kuwapa tena ufunguo wa mzinga wake wa asali.”

“Masogora wengi wamekuwa wakiomba demu huyo awarushie video kadhaa zinazoonyesha sehemu za ndani ya mapaja yake. Yaonekana ‘amewatia wengi wazimu’ na urembo wake unawafanya wengi wao kutolala kabisa!” akaongezea mdaku wa The Sun.

Japo haijulikana ni lini hasa ambapo Arabella alibwagana na De Souza, uhusiano wa kipusa huyo na Dias, 26, pia ulivunjika ghafla mwanzoni mwa mwaka huu baada ya kuchumbiana kwa kipindi kifupi kuanzia Septemba 2023.

Alipata hifadhi mpya ya penzi lake kwa Maxted kabla ya kuanza kutambaliwa na De Souza muda mfupi baadaye.

Arabella sasa ananogesha kipindi cha mahaba kwenye runinga ya ITV nchini Afrika Kusini baada ya kuaga kipindi cha ‘Love Island All Stars’ mwanzoni mwa mwaka huu.

Alipata umaarufu mnamo 2019 baada ya kujitosa kwenye ulingo wa uanamitindo.