Mpenziwe Tecra alimtishia mlinzi, mahakama yaambiwa

Mpenziwe Tecra alimtishia mlinzi, mahakama yaambiwa

Na RICHARD MUNGUTI

ALIYEKUWA mlinzi wa kibinafsi wa mrithi kampuni ya kutengeneza pombe ya Keroche Tecra Muigai alitishiwa maisha mara kadhaa na mpenziwe, Bw Omar Lali.

Bw Eric Cheruiyot aliyestaafu kutoka idara ya Majeshi ya Usalama (KDF) baada ya kuhudumu miaka sita alieleza mahakama inayochunguza kifo cha Tecra jinsi Bw Lali alimtisha wakiwa mjini Dar-es-Salaam, Tanzania na kisiwani Lamu kaunti ya Lamu 2019.

Bw Cheruiyot alimkariria kwa makini hakimu mwandamizi Bi Zainabu Abdul anayechunguza jinsi kifo cha Tecra kilivyotokea.

Mkurugenzi wa Mashtaka ya Umma (DPP) Noordin Haji aliamuru uchunguzi ufanywe ibainike ikiwa Tecra aliuawa ama alianguka na kupata jeraha kichwani lililopelekea kukata kamba kwake.

“Nilishtushwa na vitisho hivyo vya Bw Lali,” Bw Cheruiyot alisimulia.

Wakati wa kisa cha kwanza mjini Dar wakati wa sherehe za kuadhimisha siku ya kuzaliwa ya kaka yake Tecra, James Karanja, Bw Lali alipokonywa mkoba wa Tecra na Victoria (rafikiye James).

Mlinzi huyo , alisema alikabidhiwa mkoba huo na Victoria.

Victoria alimweleza Bw Lali, mwache Tecra, wewe ni Mzee na umri wako ni mkubwa, yeye ni msichana mdogo kwako.

“Matamshi hayo yalimkera , Bw Lali,” korti ilielezwa jana.

Akijibu kwa hasira, Bw Lali alimtukana mpenziwe maneno ambayo hatuwezi kuchapisha.

“Niliingilia mtafaruku huo kisha nikamweleza Bw Lali kwamba hawezi kumtukana mwajiri wangu nikiwa naye,” Bw Cheruiyot alisema.

Alimshauri Bw Lali asuluhishe tofauti zao wakiwa peke yao.

Ni wakati huo Bw Lali alimtisha mlinzi huyo na kumwambia “wewe hunifahamu nitakufanya utoweke watoto wako wasikuone tena.”

Naye Bw Cheruiyot aliumwa na matamishi hayo na kumweleza Bw Lali, “ikiwa kuna kitu unataka kufanya fanya sasa usingoje kesho.”

Usiku huo Tecra na Lali walienda bila kumwarifu Zanzibar kisha wakampigia simu.

Tecra alimtumia tikiti ya ndege akarudi Nairobi.

Akiongozwa kutoa ushahidi na wakili wa Serikali Bw Peter Muia, Bw Cheruiyot alisema kwa muda wa miezi tisa alipokuwa akifanya kazi ya kumlinda , Tecra, Bw Lali alikuwa akimtukana na kumfuruga mkurugenzi huyo wa Keroche.

Akitoa ushahidi katika uchunguzi wa kubaini kilichosaabisha kifo cha Tecra mnamo April 2020, Bw Cheruiyot alisema wapenza hao Tecra na Lwali walikuwa wanaishi maisha ya kufarakana.

Alikumbuka wakiwa katika makazi ya Tecra mjini Naivasha, alimkuta Bw Lali akilia baada ya “kufukuzwa na Tecra baada ya kuzozana usiku kucha.”

Mahakama ilielezwa wawili hao hawakuishi maisha ya amani na walizozana mara kwa mara hata wakati mmoja, Tecra alimzamba kofi Bw Lali wakiwa nje ya hoteli moja mjini Naivasha.

Uchunguzi unaendelea Alhamisi.

  • Tags

You can share this post!

Mamake Tecra jinsi mamilioni yake yalipelekewa Omar Lali

Tineja adaiwa kumuua na kumkata kichwa nyanya yake