Mpira wa Vikapu: Timu nne za Kenya zawinda taji la Red Bulls Half Court nchini Misri

Mpira wa Vikapu: Timu nne za Kenya zawinda taji la Red Bulls Half Court nchini Misri

NA RUTH AREGE

TIMU nne za mpira wa vikapu za wachezaji watatu kila upande (3×3), zinatarajiwa kuondoka nchini leo Jumatano usiku kuelekea nchini Misri kwa mashindano ya dunia ya Red Bulls Half Court.

Timu za wanawake – Elite na Dynamites ya Chuo Kikuu cha Nairobi (UoN) – na za wanaume – Tusk na Morans – zimekuwa zikifanya mazoezi katika uwanja wa Nyayo jijini Nairobi.

Timu kutoka zaidi ya nchi 20 zitawakilishwa kwenye mashindano hayo ambayo ni makubwa zaidi duniani.

Mashindano hayo yatafanyika kati ya Septemba 29 hadi Oktoba 02, 2022.

Kulingana na Naibu Mwenyekiti wa Shirikisho la Mpira wa Vikapu (KBF) Hilmi Ali, timu za Kenya zimefanya maandalizi ya kutosha kwa ajili ya mashindano hayo.

“Wachezaji wanane wa kike na wanane wa kiume wataondoka nchini chini ya mdhamini Red Bull kwa mashindano hayo. Wamejiandaa vizuri na tunatarajia wafanye vizuri,” alisema Ali.

Kocha Juma Kent ambaye hatasafiri na timu anasema maandalizi yao hayajakuwa bora zaidi lakini katika kujibu kwa haraka alisema ana imani watajitolea kwa kila kitu wanapotazama jukwaa.

Sharon Gaceri anatarajiwa kuwa nahodha wa Dynamites ambayo pia ina Faith Otieno, Alisha Ellora na Elizabeth Okumu.

Timu za wanafunzi hao ziliibuka washindi wa jumla baada ya kushindana na zaidi ya timu 30 zilizoshiriki katika mashindano ya KBF.

  • Tags

You can share this post!

Zetech Sparks yasajili watano

Yaliyojiri kabla ya Gicheru kuaga dunia

T L