Msajili wa Vyama avunjilia mbali NASA

Msajili wa Vyama avunjilia mbali NASA

Na LEONARD ONYANGO

MSAJILI wa Vyama vya Kisiasa, Ann Nderitu amevunja rasmi muungano wa National Super Alliance (NASA) uliojumuisha vyama vitano vya upinzani.

Kuvunjwa kwa muungano huo uliojumuisha Chama cha Mashinani (CCM), ODM, Amani National Congress (ANC), Ford-Kenya Party na Wiper Democratic Movement sasa kumeweka taabani nyadhifa ambazo viongozi wa upinzani walishikilia katika Bunge la Kitaifa na Seneti.

Bi Nderitu alitangaza kuvunja rasmi muungano huo baada ya kupokea barua ya kujiondoa kwa vyama vya Wiper, CCM, Ford Kenya na ANC.

Chama cha Wiper, Ford Kenya na ANC pamoja na Kanu tayari vimeunda muungano wa One Kenya Alliance (OKA) ambao haujasajiliwa rasmi na Msajili wa Vyama vya Kisiasa.

“Kifungu cha 15 (1) cha Mkataba wa Muungano kinasema muungano utavunjiliwa mbali endapo vyama vitatu vitaandika barua ya kujindoa. Kwa hiyo, muungano umevunjwa,” akasema Bi Nderitu.

Kuvunjwa kwa muungano huo kumefungua ukurasa wa kuanza mazungumzo mapya ya kuunda miungano kabla ya uchaguzi mkuu ujao. Mudavadi (ANC) na Moses Wetang’ula (FORD Kenya) kwa ajili ya Uchaguzi Mkuu wa Agosti 9, 2022.

Muungano wa NASA ulianza kukumbwa na misukosuko mnamo 2018, Bw Odinga alipofanya mazungungumzo ya kushirikiana na Rais Uhuru Kenyatta kisiri bila kufahamisha vinara wenzake.

Mabw Musyoka, Mudavadi na Wetang’ula walimtaja Bw Odinga kama msaliti.

You can share this post!

MUTUA: Afrika yafaa ijitengenezee chanjo, iache kulalamika

Kaunti 4 eneo la Magharibi kupata chanjo mpya