Msaka kazi ashtakiwa kuwapora wanabenki watatu Sh255,000 akidai atawauzia piki piki

Msaka kazi ashtakiwa kuwapora wanabenki watatu Sh255,000 akidai atawauzia piki piki

Na RICHARD MUNGUTI

MTAFUTA kazi alishtakiwa Jumanne kwa kuwafuja wafanyakazi watatu wa benki Sh255,000 akiwadanganya atawauzia piki piki.

Brian Nyamweya Makori alikana mashtaka ya kuwalaghai Martin Murage Mbaka, Evence Mchawia na Kalisto Opiyo Omondi.Makori alikabiliwa na shtaka la kumlaghai Bw Mbaka Sh115,000 mnamo Feburuari 26 2021 akidai alikuwa na uwezo wa kumuuzia piki piki almaarufu boda boda.

Bw Mbaka ni mfanyakazi katika benki ya Family Bank Limited (FBL).Shtaka la pili lilisema mnamo Machi 15 mwaka huu katika benki ya Cooperative alipokea kitita cha Sh100, 050 kutoka kwa Bw Mchawia akidai angelimuuzia boda boda.

Shtaka la tatu lilikuwa mnamo Januari 10 2021 katika benki ya Cooperative alipokea Sh40,000 kutoka kwa Bw Omondi akidai atamuuzia piki piki.Kiongozi wa mashtaka Bw Abel Omariba alimweleza hakimu mwandamizi  Bw David Ndungi kuwa kesi hiyo itaunganishwa na nyingine itakayoanza kusikizwa Agosti 17,2021.

Katika kesi hiyo mahakama ilielezwa mshtakiwa yuko nje kwa dhamana ya Sh300,000 na mdhamini mmoja.Mshtakiwa aliomba aachiliwe kwa kiwango cha chini huku akijitetea,”mheshimiwa  nilimaliza shule hivi majuzi na kamwe sina fedha za kulipia dhamana kiwango cha juu.”

Bw Ndungi alimweleza ataachiliwa tu kwa masharti sawa na mshukiwa aliyeshtakiwa awali.Kesi itatajwa baada ya wiki mbili kutengewa siku ya kusikizwa.

 

 

  • Tags

You can share this post!

Kumzuilia Ruto ni sawa na jinsi Miguna alihangaishwa, adai...

Gavana atoa onyo haitakuwa rahisi kumuondoa 2022