Msanii wa Ohangla aomba msaada

Msanii wa Ohangla aomba msaada

Na BRENDA AWUOR

MWIMBAJI maarufu wa nyimbo za Ohangla Lady Maureen Achieng, anatafuta msaada wa kutolewa hospitalini alikolazwa baada ya familia yake kumkana na kukosa kumtembelea. ?

Mwimbaji huyo ambaye amekuwa akitibiwa katika hospitali ya rufaa na mafunzo ya Jaramogi Oginga Odinga (JOORTH) kwa muda wa mwezi mmoja sasa, amekosa pa kuenda baada ya kuruhusiwa kuondoka hospitalini Februari 20.

Akiongea na Taifa Leo katika wodi yake, Bi Achieng aliomba mtu yeyote ajitokeze kumsaidia.

“Nimechoshwa na kukaa maeneo haya. Naomba msamaria mwema yeyote anitoe hapa. Bado nawapenda wote,” alisema.

Kupitia rafikiye Bi Ann Atieno, anasema kwamba mwimbaji hana pa kuenda baada ya mamake na familia yake kumkana kutokana na mzozo uliokuwa hapo awali.

Bi Atieno anaeleza kuwa mwimbaji alikuwa anaishi na mumewe maeneo ya Kendu Bay ila walikosana na akaamua kuhamia kwao Migori.

“Namfahamu Maureen kwa muda wa miaka kumi. Baada ya kukosana na mumewe alienda kwao. Lakini katika harakati za kuishi kwao, walizozana na mamake, kisa kilichofanya familia yake kumkana,” alieleza.

Haya yanatokea baada ya mmoja wa rafikize, aliyefungua akaunti ya kuchanga pesa kutoka kwa marafiki zake, kukatiza uhusiano na mwimbaji huyo.

You can share this post!

Hoja ya kuzima uuzaji muguka yaibua maoni mseto

Nzige sasa waanza kutafuna kahawa

adminleo