Habari Mseto

Mshauri wa gavana ashtakiwa kuharibu gari

August 27th, 2020 1 min read

NA Joseph Ndunda

Mshauri wa Gavana wa Laikipia Ndiritu Muriithi ambaye aliharibu gari la afisa wa UNEP ambaye anasemekana kuwa na uhusiano na mke wake, ameshtakiwa kwa uharibifu wa mali.

Isaac Githuku alishtakiwa kwa kuharibu kioo na dirisha la gari linalomilikiwa na Raymond Brandes Agosti 8.  Kijumla, aliharibu vifaa vya thamani ya Sh40,000.

Mke wake alikuwa ametoka kununua bidhaa za kutumia nyumbani kutumia gari ya Brandes na akaiegesha nje ya nyumba yao hapo ndipo Bw Githuku alienda na kuivunja vunja kulingana na stakabathi za korti.

Mkewe aliripoti kisa hicho kwenye kituo cha polisi cha Kilimani. Wawili hao walikuwa wamekutana ili wakubaliane jinsi watalea watoto. Githuku alitengana na me wake baada ya kugundua kwamba alikuwa na uhusiano na Brandes.

Watoto wake walikuwa wamemwambia kwamba mamayao alikuwa anakuja na mgeni mara kwa mara nyumbani kwake.

Bw Githuku alikataa madai hayo mbele ya jaji mkuu Derrick Kuto korti ya Kibera na kuachiliwa kwa thamana ya Sh 50,000. Kesi hiyo itatajwa tena Septemba 24.

TAFSIRI NA FAUSTINE NGILA