Kimataifa

Mshauri wa Trump kuhusu corona ajiuzulu

December 2nd, 2020 1 min read

Na MASHIRIKA

WASHINGTON D.C, Amerika

MWANASAYANSI Dkt Scott Atlas, ambaye ni mshauri wake Rais Donald Trump aliyetofautiana na wanasayansi wakuu wa kiserikali kuhusu mikakati ya COVID-19 amejiuzulu kutoka wadhifa wake katika Ikulu ya White House.

Afisa mmoja wa White House alithibitisha kwamba mtaalam huyo wa ubongo kutoka Chuo Kikuu cha Stanford, ambaye hakuwa na tajriba yoyote rasmi katika afya ya umma au maradhi ya maambukizi, alijiuzulu mwishoni mwa kazi yake ya muda serikalini.

Atlas alithibitisha habari hizo Jumatatu jioni kupitia ujumbe kwenye mtandao wa kijamii wa Twitter. Alijiunga na White House majuzi ambapo alikosoa mikakati iliyopendekezwa wataalamu Dkt Anthony Fauci na Dkt Deborah Birx.