Mshindi wa kiti cha ubunge Malindi atuliza hofu baada ya ajali iliyohusisha jamaa zake

Mshindi wa kiti cha ubunge Malindi atuliza hofu baada ya ajali iliyohusisha jamaa zake

NA MAUREEN ONGALA

ALIYEIBUKA mshindi wa kiti cha ubunge eneobunge la Malindi, Bi Amina Mnyazi, amesema jamaa na wasaidizi wake waliopata ajali mbaya barabarani wako salama.

Miongoni mwa waliojeruhiwa katika ajali hiyo iliyosababisha gari lao kuteketea, ni mtoto wake mwenye umri wa miaka miwili.

Ajali hiyo ilitokea katika eneo la Mtondia, barabara kuu ya Kilifi-Malindi usiku wa manane wa kuamkia Jumamosi.

Gari hilo lililokuwa pia na mlinzi rasmi wa Bi Mnyazi, ambaye ni afisa wa polisi, lilipata pancha kabla kubingiria mara kadha kisha kuwaka moto.

Mkuu wa Polisi wa Kaunti Ndogo ya Kilifi, Bw Jonathan Koech, alisema wote waliokolewa kabla gari kushika moto.

Bi Mnyazi hakuwa nao wakati ajali ilitokea.

“Namshukuru Mwenyezi Mungu amesimama nasi, wote wako salama. Nawaomba msiwe na wasiwasi. Mbunge wenu wa Malindi yuko salama salmini,” Bi Mnyazi akasema Jumapili.

  • Tags

You can share this post!

WANTO WARUI: Wazazi washirikishwe katika uchaguzi wa shule...

Wakazi wachagua wanaume pekee bunge la kaunti

T L