Mshindi wa kwanza wa shindano la Mozzart la Omoka na Moti ajulikana

Mshindi wa kwanza wa shindano la Mozzart la Omoka na Moti ajulikana

Na GEOFFREY ANENE

ZADOCK Sanawa kutoka Rongai ndiye mshindi wa kwanza wa shindano la kampuni ya kamari ya Mozzartbet la Omoka na Moti Promotion.

Sanawa, ambaye alipoteza kazi ya uhandisi mwanzo wa janga la virusi vya corona mwaka 2020, aliwekeza Sh50 pekee katika shindano hilo na kuvuna gari linalogharimu Sh1.2 milioni.

Washiriki 30 zaidi wa shindano hilo pia watapokea zawadi kutoka kwa kampuni hiyo mwezi huu wa likizo ya Krismasi.

Sanawa pia alitia mfukoni Sh20,827 kwa kuweka beti 14 zilizofaulu. Jina lake pia limetiwa kwenye droo ya watu 31 ambao mshindi baada ya shindano hili atajishindia nyuma mtaani Kileleshwa.

“Nimefurahi sana. Nimekosa hata la kusema. Mimi huwekeza mara kwa mara na kuishia kushinda fedha chache tu, lakini nimefurahi sana. Mimi na rafiki zangu tumekuwa tukiulizana kuwa nani ameibuka mshindi wa zawadi ya kwanza ya shindano la Omoka na Moti. Tulijadiliana na nikaweleza kuwa beti zangu zilikuwa sawa. Sikuwa nimepigiwa simu na Mozzartbet kwa hivyo sikuwa na uhakika. Nilidhani kuwa mtu mwingine ndiye mshindi,” alisema Sanawa.

Zadock Sanawa kutoka Rongai ndiye mshindi wa kwanza wa shindano la kampuni ya kamari ya Mozzartbet la Omoka na Moti Promotion. PICHA | GEOFFREY ANENE

Mchezaji mwingine alijishindia Sh15,150, ingawa aliwekeza beti 20 akitumia Sh10.

Hakutimiza sharti la kuwekeza kiasi cha chini cha kujishindia gari cha Sh50.

Mozzartbet inapanga kutuza mshindi gari kila siku aliyewekeza beti nyingi akitumia kiwango cha chini cha Sh50.

You can share this post!

Kinoti awaambia wabunge kwamba mwili wa Agnes Wanjiru...

Uhaba wa mboga dukani ulimpa kichocheo cha kujitosa katika...

T L