Michezo

Mshindi wa Supa Ligi kuamuliwa Jumapili

June 8th, 2019 2 min read

Na JOHN ASHIHUNDU

Msimu wa michuano ya Supa Ligi utamalizika Jumapili ambapo timu zote zitashiriki katika mechi za kufunga msimu huo.

Timu itakayotwaa ubingwa wa ligi hiyo pamoja na itakayomaliza katika nnafasi ya pili zitafuzu moja kwa moja hadi ligi kuu ya Kenya (KPL) inayodhaminiwa na SportPesa.

Timu itakayomaliza katika nnafasi ya tatu itakutana na Posta Rangers kuwania nafasi ya kushiriki ligi kuu msimu ujao.

Wazito ambao Jumapili watakuwa ugani Camp Toyoyo kukabiliana na St Joseph wanaongoza msimamo wa ligi hiyo kwa pointi 78, wakifuatiwa na Kisumu All Stars na Nairobi Stima ambazo kila moja inajivunia pointi 77.

Timu za Migori Youth, Green Commandos, Thika United na Kangemi All Stars zinapigania kusalia ligini baada ya kukumbwa na hali ngumu.

Wazito wanahitaji ushindi dhidi ya St Joseph ili watawazwe mabingwa wa msimu huu, mbali na kujikatia tikiti ya kushiriki ligi kuu msimu ujao.

Katika mechi zingine muhimu, Kisumu All Stars watakuwa ugenini kuvaana na Thika United ugani Thika Stadium, wakati Stima wakisuru hadi Eldoret kumalizana na Eldoret Youth katika uwanja wa Maonyesho wa Eldoret.

Shabana wanaokamata nafasi ya nane watakuwa nyumbani uwajani Gusii Stadium kupepetana na FC Talanta.

Waandalizi wa mechi hizo, Football Kenya Federation (FKF) wameamua mechi zote zianze saa nane ili kusiwe na udanganyifu.

Msimamo wa Supa Ligi ya Kenya

Namba Klabu Michezo Ushindi Sare Kushindwa Kufunga magoli Kufungwa magoli Ubora wa Mabao Alama
1 Wazito 37 25 3 9 68 35 33 78
2 Kisumu All Stars 37 22 11 4 61 28 33 77
3 Nairobi Stima 37 21 14 2 60 31 29 77
4 Ushuru 37 21 10 6 58 27 31 73
5 Kenya Police 37 18 9 10 57 50 7 63
6 Bidco United 37 17 11 9 50 36 14 62
7 FC Talanta 37 14 14 9 51 46 5 56
8 Coast Stima 37 14 10 13 49 40 9 52
9 Shabana 37 14 9 14 49 43 6 51
10 Administration Police 37 10 19 8 53 46 7 49
11 Eldoret Youth 37 12 12 13 38 46 -8 48
12 Modern Coast Rangers 37 14 6 17 44 53 -9 48
13 St Joseph Youth 37 11 11 15 45 44 1 44
14 Fortune Sacco 37 8 12 17 54 68 -14 36
15 Nairobi City Stars 37 7 15 15 45 59 -14 36
16 Kibera Black Stars 37 7 14 16 36 47 -11 35
17 Migori Youth 37 7 10 20 26 57 -31 31
18 Green Commandos 37 8 6 23 37 66 -29 30
19 Thika United 37 7 8 22 35 66 -31 29
20 Kangemi All Stars 37 8 4 25 46 78 -32 28

Ratiba ya mechi za Jumapili (zote kuanzia saa nane):

Migori Youth na Kangemi Youth (Awendo Green Stadium);

Thika United na Kisumu All Stars (Thika Stadium);

Administration Police na Bidco United (Machakos);

Wazito na St Joseph (Camp Toyoyo);

Eldoret Youth na Nairobi Stima (Eldoret Showground);

Green Commandos na Coast Stima (Bukhungu Stadium);

Kibera Black Stars na Nairobi City Stars (Hope Centre);

Shabana na FC Talanta (Gusii Stadium); na hatimaye

Kenya Police na Ushuru FC (Naivasha).